Gen Z nchini Nepal waanza mazungumzo na jeshi kutafuta kiongozi mpya

Dismas Otuke
1 Min Read

Vijana wa Gen Z nchini Nepal wanatarajiwa kuanza mazungumzo leo na viongozi wa jeshi katika jitihada za kumtafuta kiongozi mpya wa muda.

Hii ni kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika na vijana hao kupinga kukithiri kwa ufisadi serikalini mapema wiki hii, hali iliyochangia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu huku watu 30 wakiuawa katika makabiliano na polisi.

Maandamano hayo yalitochochewa na vijana hao kupitia mitandaoni, na baadaye wakateketeza bunge na afisi kadhaa za serikali.

 

Aliyekuwa Jaji Mkuu Sushila Karki, aliye na umri wa miaka, yuko kwenye mstari wa mbele baada ya wengi wa vijana hao kumpendekeza kutwaa uongozi wa taifa hilo.

Share This Article