Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu amesisitiza dhamira ya utawala wake kupanua vyuo vya kiufundi katika eneo hilo.
Ametaja vyuo hivyo kuwa muhimu katika kuwapa vijana ujuzi wa kivitendo na masoko.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano lililoandaliwa huko Nairagie Enkare, Gavana Ntutu alitoa wito kwa wazazi kuwaandikisha watoto wao, hasa wale waliokosa kujiunga na vyuo au vyuo vikuu katika kozi zinazotolewa na vyuo vya kiufundi.
Kozi zinazotolewa ni pamoja na ufundi wa mabomba, na ufundi wa magari na umeme, kozi alizosema zinawiana na viwango vya mafunzo ya umilisi.