Gavana Njuki awaonya madaktari Tharaka Nithi

Madaktari wengine wanasemekana kutekeleza majukumu yao huku wakiwataka wagonjwa kutafuta huduma za matibabu katika hospitali binafsi

Martin Mwanje
1 Min Read
Muthomi Njuki - Gavana wa Tharaka Nithi

Madaktari katika kaunti ya Tharaka Nithi wameonywa dhidi ya kutelekeza majukumu yao katika hospitali wanazofanya kazi katika kaunti hiyo, na badala yake kuwatuma wagonjwa katika hospitali binafsi kwa kisingizio kuwa huduma zinazotolewa katika hospitali za kaunti ni za kiwango cha chini. 

Gavana Muthomi Njuki anasema kuna kundi la madaktari wanaoandaa data za wagonjwa na kuwaelekeza kwa hospitali binafsi wanazomiliki kwa ahadi kwamba watapata huduma bora za matibabu.

Njuki alizungumza hayo alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya level 5 ya Chuka ili kukagua utendaji kazi wa hospitali hiyo na idadi ya madaktari wanaofika kazini kuwahudumia wagonjwa.

Gavana huyo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya afya katika Baraza la Magavana, CoG, akibaini kuwa kuna madaktari waliostahili kuwa kazini lakini hawakuonekana.

Sasa amewaonya madaktari wanaohudumu katika kaunti hiyo akionya kuwa watakaopatikana wakitelekeza majukumu yao watakiona cha mtema kuni.

Share This Article