Gavana Natembeya atoa mafahali 15 kwa familia ya marehemu Raila

Dismas Otuke
0 Min Read

Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya ametoa mchango wa mafahali 15 na magunia 15 ya mahindi kwa familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila.

Natembeya amewasilisha mchango huo siku ya Jumamosi, akiwa na wafuasi wake, nyumbani kwa Raila Kang’o katika eneo la Jarampgi, kaunti ya Siaya.

Gavana huyo ameapa kuendeleza azma na ruwaza ya hayati Raila.

Share This Article