Gavana Mutula apiga marufuku matumizi ya Plastiki Makueni

Mutula amesema hatua hii inalenga kuzuia uchafuzi wa mazingira kupitia kwa matumizi ya plastiki hizo nyepesi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Makueni, Mutula Kilonzo Junior, amepiga marufuku matumizi ya plastiki zisizotumika zaidi ya mara moja katika asifi zote za kaunti na mikutano ya maafisa wa kaunti.

Mutula amesema hatua hii inalenga kuzuia uchafuzi wa mazingira kupitia kwa matumizi ya plastiki hizo nyepesi.

Aliongeza kuwa serikali yake inalenga kujenga kiwanda cha kuyeyusha plastiki katika Manispaa ya Wote inayonakili metric tani 20 za plastiki  zinazitupwa kila siku.

Kulingana na Gavana hatua hiyo itabuni nafasi za ajira kwa vijana.

Share This Article