Katika juhudi za kukabiliana na janga la njaa Katika sehemu kame za kaunti ya Kwale serikali ya kaunti ya kwale kwa kushirikiana na ile ya kitaifa imeendeleza juhudi za kuchimba mabwawa pamoja na kuboresha miundo msingi ya maji.
Hatua hii inadhamiriwa kuhakikisha kwamba wakazi wa maeneo ya kinango na LungaLunga wanapata maji ya kutosha kuendeleza kilimo cha unyunyizi na maji ya matumizi ya nyumbani.
Gavana wa Kaunti hiyo Fatuma Achani alizundua ujenzi wa miradi mitatu ya maji huko Kinango ikiwemo ujenzi wa bwawa la wamasa kushirikiana na mamlaka ya unyunyiziaji maji mashamba nchini ,upanuzi wa mabomba ya maji katika maeneo ya moyeni na Vinyunduni huko Kinango.
Miradi ya maji ya wamasaa, moyeni na Vinyunduni inatarajiwa kufaidi takribani wakazi elfu 4000 na huduma za maji pindi itakapokamilika.