FKF yafungua maombi kwa ukufunzi wa makocha ya CAF License C

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la kandanda nchini FKF limefungua maombi ya ukufunzi ya makocha ya CAF License C.

Mafunzo hayo yataandaliwa Nakuru kati ya Aprili 7 na Juni 10 mwaka huu.

Wanaonuia kutuma maombi ni sharti wawe na stashada ya leseni ya CAF D,pia wawe makocha wanaohudumu na tajiriba ya angaa mwaka mmoja.

Mkurugenzi wa kiufundi wa FKF, Michael Amenga, amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo katika kuinua viwango vya wakufunzi wa humu nchini.

Jumla ya nafasi 30 ziko wazi kwa mafunzo hayo huku kila anayetuma maombi akihitajika kulipa ada ya shilingi 15,000, kabla ya tarehe 4 mwezi jao ambayo ni siku ya mwisho.

Share This Article