FIFA Club World Cup:PSG dhidi ya Chelsea nani atatawazwa bingwa ?

Mshindi wa kombe la leo atatuzwa shilingi bilioni 5.18, za Kenya huku timu ya pili ikitia kibindoni shilingi bilioni 3.8.

Dismas Otuke
2 Min Read

Mabingwa wa Ulaya PSG watakabiliana na Chelsea leo usiku katika fainali ya makala ya kwanza ya Kombe la Dunia baina ya vilabu yanayoshirikisha timu 32.

Fainali hiyo itakasatwa katika uwanja wa Metlife ulio jimbo la New Jersey nchini Marekani.

PSG wamepoteza mchuano mmoja pekee katika fainali za mwaka huu, bao moja kwa bila dhidi ya Botafogo, katika hatua ya makundi.

Aidha, waliongoza kundi B kwa pointi 6, baada ya kuwanyuka Atletico Madrid magoli 4-0, na kusajili mwingine wa 2-0, dhidi ya Seattle Sounders.

Katika raundi ya 16 bora, PSG waliigaragaza Inter Miami 4-0, na kuilaza Bayern Munich, 2-0, kwenye robo fainali.

Mabingwa hao wa Ufaransa walipata ushindi wa 4-0, dhidi ya Real Madrid, katika hatua ya nusu fainali.

Upande wao Chelsea walimaliza nafasi ya pili kundini D kwa alama 6, baada ya kuwashinda Los Angeles 2-0, kabla ya kupigwa na Flamengo 3-1, na hatimaye kuibwaga Esperance kutoka Tunisia 3-0.

Kwenye hatua ya 16 bora Chelsea waiipiga Benfica ya Ureno mabao 4-1, kufuatia sare ya 1-1 na kuwateam Palmeiras 2-1, katika kwota fainali.

The Blues walipata ushindi wa 2-0, dhidi ya Fluminense ya Brazil katika semi fainali.

Mshindi wa kombe la leo atatuzwa shilingi bilioni 5.18, za Kenya huku timu ya pili ikitia kibindoni shilingi bilioni 3.8.

Share This Article