Familia yadai haki kufuatia kifo tatanishi cha jamaa wao Kakamega

Martin Mwanje
1 Min Read

Familia ya mwanamume mwenye umri wa miaka 33, Raymond Nachibati, wanadai haki baada ya mwili wake kupatikana ukining’inia ndani ya seli ya kituo cha polisi cha Budonga, eneo bunge la Navakholo kaunti ya kakamega ,saa chache tu baada ya kukamatwa kufuatia mzozo wa kifamilia.

Nachibati aliripotiwa na mkewe katika kituo hicho akidai kushambuliwa, hali iliyosababisha maafisa wa usalama wa Budonga kumkamata.

Hata hivyo, familia yake ilipigwa na butwaa ilipopokea taarifa za kushtua kwamba alijitia kitanzi akiwa korokoroni.

Familia ya marehemu imesalia na maswali mengi kuhusu mazingira ya kifo chake, ikitaka kujua ni vipi mtu aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi angeweza kujitoa uhai.

Kamanda wa polisi wa eneo la Navakholo, Abdi Muhamad, amethibitisha tukio hilo kwa njia ya simu, akisema kuwa wawili hao, marehemu na mkewe, walikamatwa wakizozana katika soko la Malaha, mzozo ukiaminika kuhusiana na mke wa pili ambaye inadaiwa marehemu alikuwa ameoa.

TAGGED:
Share This Article