Kamishna Fahima Arafat Abdallah, ndiye naibu mwenyekiti wa tume huru ya mipaka na uchaguzi nchini IEBC baada ya kuchaguliw Ijumaa.
Taarifa kutoka kwa IEBC imesema kuwa makamishna sita kwa kauli moja wamepiga kura kumchagua Fahima kuwa naibu.
Makamishna hao walikutana kwenye makao makuu ya IEBC, punde baada ya kuapishwa katika mahakama ya upeo na kumchagua Fahima.
Jukumu la kwanza kwa IEBC baada ya kuapishwa siku ya Ijumaa litakuwa kuandaa chaguzi ndogo za kiti kimoja cha seneta, wabunge sita na waakilishi wadi saba.
Viti hivyo viliachwa wazi kufuatia vifo au kuchaguliwa kwa wabunge kuwa Mawaziri.