Rais William Ruto amemteua Erastus Edung Ethekon kuwa Mwenyekiti Mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, alithibitisha kuwa Rais Ruto amemteua Edung kutoka kwa orodha ya watu wawili iliyotumwa na jopo la kuwateua Mwenyekiti na Makamishna wa IEB.
Wakati huo huo, Koskei alitangaza pia Rais Ruto amewateua watakaojaza nafasi za Makamishna sita wa Tume hiyo. Walioteuliwa ni pamoja na Ann Njeri Nderitu, Moses Alutalala Mukhwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor Hassan, Francis Odhiambo Aduol, na Fahima Araphat Abdallah.
“Hatua hii ya Rais inatokana na mapendekezo ya jopo la uteuzi wa Mwenyekiti na Makamishna wa IEBC yaliyowasilishwa Jumanne 6,2025,” alisema Koskei.
Majina ya walioteuliwa na Rais, yamwewasilishwa kwa Bunge la Taifa ili kuidhinishwa kulingana na sheria za IEBC na ile ya uteuzi wa Utumishi wa Umma.