eCitizen inamilikiwa kikamilifu na serikali, asema katibu Bitok

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu wa Uhamiaji Julius Bitok.

Serikali imewahakikishia wabunge kwamba, inamiliki kikamilifu mtandao wa eCitizen ambao hutoa huduma za serikali kidijitali.

Katibu wa idara ya uhamiaji Julius Bitok, aliambia kamati ya bunge la taifa kuhusu usalama wa taifa kwamba serikali pia inahifadhi stakabadhi zote zinazothibitisha inamiliki eCitizen.

Bitok alifahamisha kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Narok Magharibi  Gabriel Tongoyo kwamba, serikali haifichi umiliki wa eCitizen pamoja na mitakaba ilitia saini na wadau wengine kupiga jeki operesheni za kiufundi.

“Ninathibitisha kuwa kuna mkataba ulioidhinishwa ma Mwanasheria Mkuu na kutiwa saini na halmashauri ya habari na Teknolojia (ICTA). Mkataba huu unathibitisha kuwa eCitizen inamilikiwa kikamilifu na serikali,” alisema katibu huyo.

Aidha alisema kuwa kufuatia agizo la Rais William Ruto ya mwaka 2024 kwamba raia wa kigeni hawahitaji viza kuingia hapa nchini, idadi ya wageni wanaozuru tafa hili imeongezeka kwa asilimia 20.

Katibu huyo alikuwa ameandamana na Mkurugenzi Mkuu wa eCitizen Isaac Ochieng na mwenzake wa uhamiaji Evelyn Cheluget, miongoni mwa wengine.

Share This Article