Tume ya maadili na kupambana na rushwa nchini EACC, imerejesha vipande 12, vya ardhi vya thamani ya shilingi milioni 320, iliyokuwa imenyakuliwa na matapeli katika kaunti za Bungoma na Kakamega.
Ardhi hiyo inajumuisha nyumba za serikali na ardhi ilinyakuliwa na wastawishaji wakibinafsi kwa kushirikiana na maafisa wa umma.
Tume hiyo pia inafuatilia vipande vingine 56, iliyonyakuliwa kwa njia haramu inayomilikiwa na mashirika ya serikali ikiwemo idara ya nyumba,Mahakama,mamlaka ya safari za angani, shirioka la reli na hazina kuu katika eneo la magharoibi ya Kenya.
Akizungumza Mumias kwenye kikao kilichohudhuriwa na maafisa wa kaunti za eneo la magharibi zikiwemo Kakamega, Busia, Bungoma,na Vihiga meneja wa EACC, eno la magharibi Eric Ngumbi, alihoji ongezeko la unyakuzi wa ardhi ya serikali katika eneo hilo.
Aliwataka Machifu na maafisa wengine wa utawala kujiunga katika vita dhidi ya ufisadi.