Duale: Wizara haina uwezo wa kuajiri wahudumu wa afya ya jamii kwa masharti ya kudumu

Duale alikuwa akizungumza katika hafla moja ya kitamaduni huko Garissa.

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa Afya Aden Duale amesema kwamba wizara hiyo haina uwezo wa kifedha kuajiri wahudumu wa Afya wa jamii kwa masharti ya kudumu.

Akijibu maswali ya Maseneta kuhusu maslahi ya wahudumu hao katika tamasha la kitamaduni huko Garissa, aliwataka maseneta watenge pesa kwenye bajeti za kulipa mishahara ya wahudumu hao.

Masuali hayo yaliibuliwa na Seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna na mwenzake wa Vihiga Godfrey Osotsi.

Waziri huyo aliendelea kusema kwamba pesa zilizopo ni bilioni 3.5 pekee ambazo zinaweza kutumika kuajiri wauguzi kwa mikataba isiyo ya kudumu.

Kulingana na waziri huyo, mishara ya wauguzi na wahudumu wa afya wa jamii ambao wametia saini mikataba ya ajira itahamishiwa kaunti zao.

Haya yanajiri wakati ambapo wahudumu hao wa afya wa jamii wametishia kuendelea kugoma hadi wakati ambapo matakwa yao yatatimizwa na serikali.

Wanataka waajiriwe kwa masharti ya kudumu na walipwe hela zao za baada ya kukamilika kwa mkataba wa kikazi.

Share This Article