Duale kutoa orodha ya hospitali zilizoshiriki ufisadi na NHIF

Tom Mathinji
2 Min Read
Waziri wa Afya Aden Duale kutoa orodha ya hospitali bandia hapa nchini.

Waziri wa Afya Aden Duale ametoa onyo kali kwa vituo bandia vya afya, akisema kuwa hatasita kutoa orodha ya hospitali bandia ambazo zilishiriki shughuli za ufisadi na iliyokuwa Hazina ya Kitaifa ya Afya (NHIF).

Aidha waziri huyo aliazimia kutekeleza msako dhidi ya matabibu bandia, akitoa wito kwa wadau wote wa sekta ya Afya kuhudumu kwa kuzingatia sheria. Alisema hatua hiyo ni  muhimu katika utekelezaji wa Huduma ya Afya kwa Wote  (UHC).

Waziri huyo alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mkakati wa ushirikiano mpya  kati ya wizara ya Afya na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan.

Ushirikiano huo utapiga jeki matibabu ya operesheni, ikiwemo upandikizaji wa figo, oparesheni za moyo kupitia Halmashauri ya Afya ya Jamii (SHA). Ushirikiano huo unalenga kuhakikisha Wakenya wanapata huduma za dharura za Afya.

“Ushirikiano huu ni muhimu katika kupunguza gharama ya matibabu, hususan kwa walio katika hatari ya kuambukizwa. Hakuna Mkenya anapaswa kukoksa huduma za dharura za Afya kwa sababu ya ukosefu wa hela,” alisema Duale.

Waziri huyo alitoa wito kwa vituo vingine vya matibabu, vile vya umma, kibinafsi na vinanyomilikiwa na taasisi za kidni, kusaidia katika

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan Dkt. Sulaiman ShahbuddinAfisa Mkuu mtendaji wa hospitali hiyo Rashid Khalani, katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni, Afisa MKuu mtendaji wa SHA Dkt. Abdi Mohamed, na maafisa wengine wakuu katika wizara ya Afya.

TAGGED:
Share This Article