Waziri wa Afya Aden Duale, amebuni kamati ya watu 13 kuchunguza madai ya ulanguzi wa viungo vya mwili katika hospitali za Mediheal.
Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali, kamati hiyo itaongozwa na professa Elizabeth Bukusi wakati afisi kuu ikiwajumuisha Stella Kanja, Rueben Tulei, na Jedidah Effie Oduor.
Kmati hiyo itachunguza sharia zilizopo za kuthibiti huduma ya upachikaji wa viungo vya mwili na jinsi hospitali za Mediheal zilivyokiuka sheria hizo.
Uchuanguzi huo unafuatia ripoti kutoka shirika la utangazaji la Deutsche Welle iliyoadai kuwa hospitali za Mediheal zimekuwa zikihiriki katika ulanguzi mkubwa wa viungo vya binadamu.