Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza zawadi ya dola milioni 5 sawa na shilingi milioni 650 za Kenya, kwa yeyote atakayetoa habarai zitakazosaidia kukamtwa kwa viongozi watatu wakuu wa kundi la wanamgambo wa M23.
Viongozi hao wa M23 wanaowindwa ni pamoja na aliyekuwa msimamizi mkuu wa tume ya uchaguzi Corneille Nangaa, Kamanda wa jeshi Sultani Makenga, na kiongozi wa kisiasa Bertrand Bisimwa.
Watatu hao walikuwa walihukumiwa kunyongwa mwaka jana kwa kosa la uhaini.
Rais Felix Tshisekedi, ameitaka jamii ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuunga mkono kundi hilo la M23, ambalo limenyakua miji kadhaa nchini Congo ikiwemo Goma na Bukavu huku maelfu ya watu wakiuwa na wengine kufurushwa makwao.