Rais Felix Tsishekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesisitiza kuwa serikali yake itakabiliana vikali na kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda.
Tshisekedi amesema atatuma majeshi yake kuwazima M23 ambao wamethibiti mji wa Goma mashariki mwa nchi hiyo wenye madini mengi.
Waasi wa M23 wametwaa maeneo mengi ya mji wa Goma ulio makao makuu ya mkoa wa Kivu Kaskazini.
Tshisekedi alisusia mkutano wa jumuia ya Afrika- EAC, uliohudhuria na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mapema wiki hii.
Wanajeshi 13 waliokuwa sehemu ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Maendeleo Kusini mwa Afrika (SAMIDRC),
wameuawa na waasi wa M23 .