Congo na Rwanda zimewasilisha muswada wa mapendekezo ya pamoja yanayolenga kumaliza mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Muswada huo uliosainiwa leo Jumatatu mbele ya maafisa wa serikali ya Marekani, unalenga kukomesha vita huu serikali ya Marekani ikiahidi kuwekeza mabilioni ya dola nchini humo.
Hatua hii ni ya hivi punde ya serikali ya Marekani yake Donald Trump, kujaribu kumaliza mzozo huo wa miongo kadhaa nchini Congo DR.
Mapigano mashariki wa DRC kati ya majeshi ya serikali na waasi wa M23 wanaokisiwa kufadhiliwa na serikali ya Rwanda yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu nchini humo.