Mkurugenzi wa Mashtaka Umma (DPP), nchini Tanzania, ameondoa kesi ya uhaini dhidi ya mfanyabiashara wa vipodozi Jenifer Jovin maarufu Niffer, na Mika Lucas Chavala, huku mahakama ikiwaachilia huru.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Desemba 3, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu Dr es Salaam, baada wakili wa Serikali, kuileleza Mahakama hiyo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Jeniffer Jovin mwenye umri wa miaka 26 pamoja na Mika Chavala walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhaini.
Ikumbukwe Novemba 25, 2025 washtakiwa 20 kati ya 22 ambao walikuwa wanashtakiwa pamoja na Niffer waliachiliwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka yao.