Dkt. Ronoh: Ushirikiano wa Kenya na Italia umepiga jeki ukuaji wa uchumi

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu katika wizara ya kilimo Dkt. Kipronoh Ronoh ashauriana na maafisa wa ngazi za juu kutoka Italia

Katibu katika wizara ya kilimo Dkt. Kipronoh Ronoh, alifanya mazungumzo na ujumbe kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kutoka Italia, ukiongozwa na balozi wa Italia hapa nchini Roberto Natali.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Ronoh alipongeza Italia kwa kuunga mkono miradi ambayo inapiga jeki ukuaji wa uchumi wa taifa hili, hususan katika maeneo kame hapa nchini.

Kulingana na katibu huyo, shirika la maendeleo la Italia hapa nchini hutekeleza miradi katika sekta ya kilimo na mazingira katika maeneo kame kama vile Pokot Magharibi, Baringo na Kilifi.

“Italia ni miongoni mwa washirika wa Kenya wa jadi, huku miradi mingi ya maendeleo ya kilimo ikitekelezwa kupitia ushirikiano huo. Tunapongeza ukuaji wa ushirikiano huu kati ya nchi hizi mbili,” alisema Dkt. Ronoh.

Dkt. Ronoh aliongeza kuwa miradi inayotekelezwa na Itali hapa nchini, inawiana na ajenda ya ukuaji wa uchumi wa taifa hili kutoka chini almaarufu BETA.

“Miradi hiyo inayotekelezwa inawiana na ajenda ya serikali ya Rais William Ruto ya Bottom-up Economic transformation Agenda (BETA) na ruwaza ya Kenya ya mwaka 2030”, aliongeza Dkt. Ruto.

Share This Article