Dkt. Gilda Odera ateuliwa naibu mwenyekiti wa SRC

Tom Mathinji
1 Min Read
Dkt. Gilda Odera.

Tume ya kuratibu mishahara na marupurupu SRC, imemteua Dkt. Gilda Odera kuwa naibu mwenyekiti wake.

Kupitia kwa taarifa siku ya Ijumaa, tume hiyo ilidokeza kuwa uteuzi wa Dkt. Odera utaimarisha majukumu ya tume hiyo ya kubuni na kufanyia marekebisho mishahara ya watumishi wa umma.

“Tume hii inampongeza Dkt. Gilda Odera kufuatia uteuzi wake, na inamtakia ufanisi anapoanza kutekeleza majukumu yake,” ilisema SRC kupitia kwa taarifa.

Huku akiwa na tajiriba ya miaka 30 katika usimamizi, Odera amehudumu wadhifa wa afisa mkuu mtendaji, mkurugenzi wa bodi na kiongozi wa maswala ya sera katika viwango tofauti.

Dkt. Odera ambaye anawakilisha chama cha waajiri katika tume hiyo, anashahada ya uzamili katika somo la kijamii kutoka chuo kikuu cha Nairobi, uzamifu katika ubunifu na mabadiliko kutoka chuo kikuu cha York St. John nchini Uingereza.

Kabla ya uteuzi huo, Odera alihudumu kama mwanamke wa kwanza Rais wa chama cha waajiri nchini FKE.

Share This Article