Diddy amewasilisha barua kwa mahakama akiomba ahurumiwe huku akiomba msamaha kwa watu wote ambao aliumiza na kuwajibikia makosa yake.
Msanii huyo anatarajiwa kuhukumiwa leo na tayari watu wa familia yake wamefika mahakamani na Jaji Arun Subramanian naye tayari ameingia mahakamani.
Watu wa familia yake walionyesha nyuso zenye huzuni walipokuwa wakiingia mahakamani wakiongozwa na mamake Diddy kwa jina Janice ambaye amevaa mavazi ya rangi nyeupe.
Mwanawe Diddy aitwaye Christian Combs na mpenzi wake aitwaye Raven Tracy waliingia mahakamani pamoja, wakifyatiwa na Quincy Brown, Jessie Combs, D’Lila Combs na Chance Combs waliotembea kwenye foleni wakiingia mahakamani.
Mzazi mwenza wa Diddy aitwaye Dana Tran naye yupo mahakamani na amevaa mavazi ya rangi nyeusi. Tran hata hivyo hakuwa na mtoto wao wa kike ambaye ni mdogo kabisa kati ya watoto wa Diddy.
Upande wa mashtaka tayari umeashiria kwamba ungependa msanii huyo ahukumiwe kifungo cha miaka 11 gerezani huku mawakili wake wakitaka afungwe miezi 14 pekee na muda aliokaa kizuizini uzingatiwe.
Mawakili wa Diddy wanatarajiwa kuonyesha mahakama video ya dakika 12 ya kuonyesha jukumu la Diddy katika jamii kama njia ya kumtetea asifungwe muda mrefu.