Diamond asema yeye ni mume wa mtu

Alisema hayo jukwaani alipokuwa akitumbuiza huku uvumi ukisambaa kwamba tayari ameshatoa talaka kwa Zuchu aliyefunga naye ndoa.

Marion Bosire
2 Min Read

Siku chache baada ya kuachia picha za ndoa yake na Zuchu, Diamond sasa amejirejelea kama mume wa mtu.

Msanii huyo wa Tanzania alikuwa jukwaani akitumbuiza kwenye mkesha wa mwenge ilala usiku wa kuamkia leo ambapo alisimamisha muziki kwa muda na kusema yeye sasa ni mume wa mtu.

“Niwambie kitu, siku ya leo… Mimi sikuwa vizuri kwenye afya, nilikuwa najiskia kuumwa Umwa,unajua ukishakuwa ndani ya ndoa… kuna ka namna yani…. mi mume wa mtu jamani mjue.. nina kazi maalumu muda huu” alisema msanii huyo kabla ya kurejelea burudani.

Zuchu naye amebadilisha wasifu wake kwenye akaunti yake ya Instagram na kuongeza kwamba yeye ni mke wa Diamond Platnumz ila hajarejesha maelezo aliyoondoa ya kuonyesha kwamba yuko chini ya kampuni ya WCB.

Alichapisha pia video ya Diamond akidai kuwa mume wa mtu kwenye Insta Stories na kuandika, “Mume wangu mimi”.

Hata ingawa wawili hao wanaonekana kurushiana maneno ya mapenzi inaripotiwa kwamba picha walizochapisha ni za ndoa iliyofungwa mwezi wa nne na wala sio juzi.

Mange Kimambi anadai kwamba Zuchu alitaka kwa lazima aolewe na Diamond la sivyo ajitoe uhai na hivyo Diamond akalazimika kumwoa pasi na ufahamu wa watu wa familia yake.

Kulingana na Mange, Diamond alitoa talaka tatu kwa pamoja kwa Zuchu siku tatu kabla ya harusi ya Juma Jux lakini zimehesabiwa kama moja kwani hazifai kutolewa kwa pamoja.

Baba Levo ambaye humrejelea Diamond kuwa mzazi wake aliandika kwenye Instagram kwamba, “Sasa nimegundua talaka moja haina nguvu asanteni wazazi wangu mmeniheshimisha”.

Share This Article