Dhuluma za kijinsia zaongezeka Yatta, Machakos

Martin Mwanje
1 Min Read

Asasi za usalama zimetakiwa kuwajibikia kwa kina usalama katika eneo la Yatta hususan mjini Matuu, ambapo visa vya mauaji kwenye ndoa au mahusiano vimeripotiwa kuongezeka katika siku za hivi  maajuzi. 

Kwa muda wa mwezi mmoja umepita, zaidi ya wanandoa 4 wamepoteza maisha yao katika visa tofauti katika eneo hilo kutokana na dhulma za kimapenzi, na sasa viongozi wa kidini eneo hilo wanaitaka serikali kuchukua hatua madhubuti za kiusalama na uchunguzi wa kina kufanyika ili kuwawajibisha wahusika.

Wachungaji Fidelis Masila na Reuben Muindi kutoka kanisa la AIC Matuu wanasema ni jambo la kusikitisha kuona wanandoa wachanga wakipoteza maisha yao kutokana na hali zisizoeleweka na ni pigo kwa jamii husika na kanisa kwa jumla.

Aidha, wamelauumu wanandoa kwa kuiga hulka za mitandao wanazosema zimechangia kwa kiwango kikubwa mauaji ya sasa na kusema kwamba ndoa nyingi zinakabiliwa na tishio la kuvunjika.

Pia wanawalaumu maafisa wa polisi eneo hilo kwa kuzembea kuchunguza visa mbalimbali ambavyo vimekuwa vikiripotiwa kikiwemo kisa cha juzi ambapo afisa wa polisi kutoka Kanyonyoo aliwapiga risasi na kuwauwa wanawake wawili.

Share This Article