D4vd akiri mapenzi yake kwa mtu aitwaye Celeste katika wimbo

Marion Bosire
2 Min Read
Mwanamuziki D4vd

Katika wimbo wa mwanamuziki D4vd ambao umevujishwa, anasikika akikiri mapenzi yake kwa mtu aitwaye Celeste, jina linalofanana na msichana wa umri wa miaka 15 ambaye mwili wake ulipatikana ukioza kwenye gari lake.

Baadhi ya maneno kwenye wimbo huo ni kama, “”Oh, Celeste / Msichana aliyechora jina langu kwenye kifua chake / Ninamnusa kwenye nguo zangu kama sigara/ ninasikia sauti yake kila ninapopumua/ Amanishika.”

Ulipovujishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2023, wimbo huo ulikuwa unaitwa “Celeste_Demo unfin”.

Mamake Celeste Rivas, ambaye mwili wake uliokuwa umekatwa katwa na kuoza ulipatikana ndani ya tesla ya D4vd aliambia wanahabari kwamba binti yake alipotea Aprili 2024 na alikuwa na mpenzi aitwaye David.

Hata hinyo haijabainika iwapo Celeste aliyeimbwa ni yule aliyepatikana kwenye gari hilo kwa jina Celeste Rivas lakini iwapo ni yeye inamaanisha kwamba walijuana vyema na mwanamuziki huyo hata kabla yake kutoweka.

Haya yanajiri kufuatia siku kadhaa za uchunguzi wa maafisa wa polisi baada yao kufahamishwa kuhusu uvundo mbovu uliokuwa ukitoka kwenye gari hilo linalomilikiwa na D4vd.

Gari hilo lilikuwa kwenye maegesho ya magari yaliyotwaliwa kwa sababu mbali mbali huko lake likiletwa huko baada ya kutelekezwa huko Hollywood.

Wakati wa kupatikana kwa gari hilo mwanamuziki huyo alikuwa anaendeleza ziara yake ya kikazi.

Ilibainika pia kwamba binti huyo alikuwa na mchoro kwenye kidole unaofanana na ulio kwenye kidole cha D4vd.

Share This Article