Copa America: Marekani na Uruguay kumenyana

Martin Mwanje
1 Min Read

Marekani ambao ni wenyeji wa kipute cha Copa America watakabana koo na Uruguay saa tisa usiku katika mechi ya mwisho ya kundi C sawia na Panama dhidi ya Bolivia.

Hadi sasa, Uruguay wanaongoza kundi hilo kwa alama sita. Marekani ni ya pili kwa alama tatu sawia na Panama ila zinatofautiana kwa idadi ya magoli zilizofungwa huku Bolivia wakiburura mkia bila alama.

Hivyo, ili waandalizi hao wafuzu kwa robo fainali, lazima washinde kwa magoli mengi. Pia, wanaweza kufuzu kupitia sare kutegemea matokeo ya Panama.

Mapema leo kwenye mechi za mwisho za kundi B, Venezuela waliilaza Jamaica mabao matatu kwa bila kupitia Eduard Bello, Salomón Rondón na Eric Ramírez mnamo dakika za 49, 56 na 85 mtawalia.

Mexico na Ecuador walitoka sare ya yai kwa yai. Baada ya mechi za kundi hilo kukamilika, Venezuela na Ecuador zimefuzu kwa robo fainali kwa alama tisa na nne mtawalia.

Ecuador na Mexico zimeaga mashindano.

Share This Article