Coe, apongeza juhudi za Kenya kupambana na ulaji muku

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa shirikisho la Riadha ulimwenguni, Sebastien Coe, amepongeza juhudi zilizopigwa na Kenya katika kukabiliana na ulaji muku.

Coe alisema haya jana jioni kwenye kikao na Wanahabari kilichoandaliwa katika afisi za chama cha Riadha Kenya.

Coe hata hivyo, alisema kutokana na idadi kubwa ya wanariadha wa Kenya wanaoshiriki mashindanoni, taifa hili litasalia katika kundi la kwanza la nchi zinazochunguzwa zaidi kwa matumizi ya dawa za kututumua misuli.

Kinara huyo ambaye alikuwa nchini kwa ziara ya siku moja pia alikutana na Rais William Ruto jana jioni, kabla ya kuondoka.

Coe anawania Urasi wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC), katika uchaguzi wa tarehe 16 mwezi huu.

Share This Article