Chui watafunwa Awendo na limbukeni Mara Sugar

Dismas Otuke
1 Min Read

Rekodi ya klabu ya AFC Leopards ya kutoshindwa msimu huu ligini imefikia tamati Jumamosi baada ya kuambulia kichapo cha magoli 2-0, ugenini dhidi ya Mara Sugar inayoshiriki ligini kwa mara ya kwanza.

Nguvu mpya Dennis Cheruiyot alipachika magoli yote mawili kwa Mara kunako dakika za 88 na 94 wakisajili ushindi wa pili ligini.

Kwenye matokeo mengine Nairobi United wameichachafya  Kariobangi Sharks mabao 4-2, katika uwanja wa Dandora na kuchupoa hadi nafasi ya tatu ligini kwa pointi 12.

Share This Article