Mabingwa mara mbili wa kombe la CHAN Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,walisajili ushindi wa kwanza katika fainali za mwaka huu baada ya kuwacharaza Zambia mabao 2-0, Alhamisi jioni katika uwanja wa Nyayo.
Ibrahim Matobo Mubalu aliwaweka Congo uongozini dakika ya 51, kabla ya Malanga Horso Mwaku, kuongeza la pili dakika ya 71.
Ilikuwa ni afueni kwa Congo baada ya kushindwa na Kenya bao 1 kwa bila katika mchuano wa ufunguzi.