Mabingwa mara mbili wa kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), DR Congo, maarufu kama the Leopards, wamewasili mapema Alhamisi tayari kushiriki kipute cha mwaka huu.
Chui wa Congo wamekuwa kwenye kambi ya mazoezi jijini Dar es Salaam, Tanzania, tangu mwishoni mwa wiki jana kujiandaa kwa kipute cha CHAN, wakijiuvunia kutawazwa mabingwa mwaka 2009 na 2016.
DRC watafungua mechi za kundi A Jumapili hii dhidi ya wenyeji Harambee Stars ya Kenya katika uwanja wa Kasarani.
Timu nyingine kundini A ni Congo, Morocco, Angola, na Zambia.