Chipukizi wa Uganda waigutusha Ufaransa na kufuzu kwa raundi ya 32, Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Uganda kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 imefuzu kwa raundi ya 32 bora katika fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar.

Uganda imesajili ushindi wa bao moja kwa nunge dhidi ya Ufaransa katika mechi ya mwisho ya kundi K.

Ushindi huo umeiwzesha Uganda kumaliza ya tatu kundini humo kwa alama 4 huku kila timu ikikamilisha ratiba ya mechi za makundi kwa alama sawa 4.

Uganda inajiunga na mataifa mengine ya Afrika yaliyofuzu kwa raundi ya pili yakiwemo Mali, Burkina Faso, Zambia, Afrika Kusini, Morocco, Senegal, Tunisia, na Misri.

Share This Article