China yasema inataka ‘kuimarisha ushirikiano’ katika mazungumzo ya biashara na Marekani

Martin Mwanje
1 Min Read
Lan Fo'an - Waziri wa Fedha wa China

China ilisema leo Jumatano kuwa itatafuta “kuimarisha ushirikiano” na Marekani kwenye mazungumzo ya biashara ya wiki ijayo mjini Stockholm nchini Uswidi.

“Kwa misingi ya usawa, heshima na manufaa ya pande mbili… tutaimarisha makubaliano, kupunguza kutoelewana, kuimarisha ushirikiano na kuhamasisha maendeleo thabiti, mazuri na endelevu ya uhusiano kati ya China na Marekani,” amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Guo Jiakun.

Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent alisema jana Jumanne kwamba atakutana na mwenzake wa China mjini Stockholm wiki jayo kwa ajili ya mazungumzo ya ushuru wa forodha, akilenga uongezaji wa muda wa mwisho wa mazungumzo hayo hadi katikati ya mwezi Agosti mwaka huu.

 

TAGGED:
Share This Article