Waziri Mkuu wa China Li Qiang ametangaza kuanza kwa ujenzi wa bwawa kubwa zaidi la kuzalisha umeme duniani, kwenye ukingo wa mashariki wa Tibet, kwa gharama inayokadiriwa dola bilioni 170, limesema shirika rasmi la Xinhua.
Bwawa hilo litakalokuwa na vituo vitano vya kufua umeme litazalisha kilowati bilioni 300 za umeme kila mwaka, sawa na kiasi cha umeme kilichotumiwa na Uingereza yote mwaka jana.
India na Bangladesh tayari zimeibua wasiwasi juu ya uwezekano wa athari za bwawa hilo kwa mamilioni ya watu chini ya mto, huku NGOs zikionya juu ya hatari kwa mazingira.
Beijing imesema bwawa hilo litasaidia kukidhi mahitaji ya nishati huko Tibet na maeneo mengine ya China bila kuleta athari kubwa kwenye usambazaji wa maji ya mto au mazingira.
Litarajiwa kuanza kufanya kazi wakati fulani katika miaka ya 2030.