Bingwa wa New York City Marathon, Purity Chepkirui, atashiriki makala ya mwaka huu ya mbio za wanawake za Nagoya zitakazoandaliwa Jumapili hii nchini Japan.
Chepkirui mwenye umri wa miaka 34, alianza kushiriki mbio za marathon mwaka 2022 mjini Valencia, kabla ya kukimbia London na Berlin marathon.
Mwaka uliopita aliandikisha ushindi wake mkubwa alipotwaa ubingwa wa New York City Marathon kwa muda wa saa 2 dakika 24 na sekunde 35.
Chepkirui ndiye mwanariadha mwenye kasi katika mbio za Jumapili, huku akishindana na Ruti Aga wa Ethiopia na Eunice Chumba wa Bahrain.
Wanariadha wapatao 20,000 wametoa ithibati kushiriki mbio za Jumapili.