Bingwa wa mwaka jana katika mbio za New York City Marathon Sheila Chepkirui, ameshinda makala ya mwaka huu ya mbio za wanawake za Nagoya mapema leo nchini Japan.
Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 34 alisajili ushindi wa pili mtawalia katika amali yake ya marathon kwa kusajili muda wa saa 2 dakika 20 na sekunde 40 ,sekunde 19 mbele ya Sayaka Sato wa Japan, huku mzaliwa wa Kenya raia wa Bahrain Eunice Chumba,akimaliza wa tatu kwa saa 2 dakika 21 na sekunde 35.
Chepkirui amezawadiwa shilingi milioni 32.5 za Kenya kufuatia ushindi huo.