Chepkemoi na Kemboi waongeza dhahabu za Kenya, Riadha ya chipukizi Afrika

Kemboi aliongeza dhahabu ya mita 5000 kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 akiziparakasa kwa dakika 13 sekunde 22.81.

Dismas Otuke
1 Min Read

Claire Chepng’etich  Denis Kemboi walinyakua medali za dhahabu Jumamosi usiku katika siku ya nne ya makala ya tatu ya mashindano ya riadha ya Afrika kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18 na miaka 20, katika uwanja wa Mashood Abiola mjini Abeokuta,Nigeria.

Chepng’etich alinyakua dahahabu katika fainali ya mita 2,000 kuruka viunzi na maji  kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18, akitumia dakika 6 sekunde 33.2 ,huku Mercy mageso pia wa Kenya akishinda shaba.

Kemboi aliongeza dhahabu ya mita 5000 kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 akiziparakasa kwa dakika 13 sekunde 22.81.

Mashindano hayo yatakamilika Jumapili usiku huku  .

Share This Article