Loice Chemining wa huduma za Magereza, ndiye bingwa mpya wa mita
10,000, katika mashindano ya kitaifa ya riadha yaliyoanza leo katika
uwanja wa Ulinzi Complex.
Chemining ambaye pia ni bingwa wa magereza, alitawala mbio hizo na kukata
utepe wa kwanza kwa dakika 31 sekunde 22.39.09,akifuatwa na Cintia
Chepnge’no wa KDF kwa dakika 32 sekunde 22.44, huku Rebecca Mwangi wa
Magereza akihitimisha nafasi tatu bora.
Mary Nyaruai wa Police aliibuka mshindi wa mita 1500, kwa kutumia muda
wa dakika 4 sekunde 09.68, akifuatwa na bingwa wa zamani wa dunia
kwa chipukizi Teresia Gateri kutoka Central na Vivian Kiprotich wa
KDF katika nafasi za pili na tatu mtaliwa.
Mashindano hayo yatakamilika Ijumaa ,yakiwa mashindano ya mwisho ya uwanjani msimu huu.