Chelsea ndio mabingwa wa kombe la Dunia baina ya vilabu mwaka huu baada ya kuwazidi maarifa PSG walipowanyuka mabao 3-0 kwenye fainali ya jana Jumapili usiku ugani Metlife katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.
Cole Palmer alipachika mabao mawili huku Joao Pedro akiongeza moja katika kipindi cha kwanza kuhitimisha ushindi huo maridhawa.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa Mabingwa hao wa Ulaya kupoteza kwenye fainali ya Kombe hilo la Dunia tangu mwaka 2012, wakati Chelsea iliposhindwa na Corinthians.
Cole Palmer alitawazwa mchezaji bora, Robert Sanchez akatuzwa kipa bora huku Desire Doue wa PSG, akishinda tuzo ya mwanandinga chipukizi bora.
Chelsea walitia kibindoni shilingi bilioni 5.1 kwa ushindi huo huku PSG wakituzwa shilingi bilioni 3.8.