Chelsea watachuana na mimba wa Brazil Palmeiras katika robo fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu nchini Marekani.
Chelsea ilihitaji muda wa ziada ili kuwashinda Benfica kutoka Ureno mabao 4-1 ,kufuatia sare ya bao moja ndani ya dakika 90.
Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Bank of America eneo la North Carolina, na ilisitishwa kwa takriban saa 2 punde baada ya radi kushuhudiwa kilomita 30 kutoka uwanjani kunako dakika ya 84.
kwa kawaida wataalam wa hali ya anga maeneo yaliyo karibu na bahari wemeshauri wachazeji na mashabiki kuondoka uwanjani kwa dakika 30 kila kunapoonekana dalili na radi.
Chelsea walichukua ongozi kunako dakika ya 64 kupitia kwa nahodha Reece James,kabla ya Angel Di Maria, kusawazishia Benfica katika dakika ya 95.
Hata hivyo Christopher Nkunku,Pedro Neto na Kiernan Dewsbury-Hall, walifunga bao moja kila mmoja katika dakika za 108,114 na 117 mtawalia na kuwapa Chelsea ushindi.
Katika mechi ya kwanza ya raundi ya 16 bora Palmeiras walihitaji goli la muda wa ziada la dakika ya 100 lake Paulinho liliwapa ushindi dhidi ya mabingwa wa Botafogo.
Palmeiras na Chelsea zitakabiliana Julai 5 katika uwanja wa Lincoln Financial Field mjini Philadelphia.