Chebet atwaa dhahabau ya kwanza kwa Kenya huko Tokyo

Chebet ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki katika shindano hilo aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa dakika 30  sekunde 37.61.

Dismas Otuke
1 Min Read

Beatrice Chebet alistahimili ukinzani mkali kabla ya kuishindia Kenya dhahabu ya kwanza ya mita 10,000 katika siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha Ulimwenguni mjini Tokyo, Japan.

Chebet ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki katika shindano hilo aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa dakika 30  sekunde 37.61.

Mwitaliano Nadia Batocletti, alinyakua fedha kwa dakika 30 sekunde 38.23 ,huku bingwa wa mwaka 2023 Gudaf Tsegay wa Ethiopia aliyeshinda shaba kwa dakika 30 sekunde 39.65.

Chebet ndiye Mkenya wa kwanza kunyakua dhahabu ya mbio hizo tangu Vivian Cheruiyot mwaka 2015.

Aidha, mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 24 atashiriki fainali ya mita 5,000 wakishirikiana na bingwa mtetezi Faith Kipyegon, Margaret Akidor na Agnes Jebet Ngetich.

Share This Article