Chebet akosa sekunde 2.5, avunje rekodi ya dunia ya mita 5,000

Chebet aliziparakasa mbio hizo kwa muda wa dakika 14 sekunde 3.69

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Olimpiki Beatrice Chebet, alikosa sekunde mbili unusu ,kuvunja rekodi ya dunia ya mita 5000, katika mashindano ya Golden Gala Diamond League, Ijumaa usiku mjini Rome, Italia.

Chebet aliziparakasa mbio hizo kwa muda wa dakika 14 sekunde 3.69, akisajili muda wa kasi wa pili katika historia pamoja na kuvunja rekodi ya kitaifa, akikaribia rekodi yake Gudaf Tsegay wa Ethiopia ya dakika 14 nukta 21.

Freweyni Hailu wa Ethiopia, alimaliza wa pili kwa dakika 14 sekunde 19.33, huku Mwitaliano Nadia Batocletti, akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 14:23.15.

Bingwa wa dunia mwaka 2019, Timothy Cheruiyot wa Kenya, alimaliza wa pili katika mita 1500 kwa muda wa dakika 3 sekunde 29.75, nyuma ya Mfaransa Nadsine Habb, aliyetwaa ushindi kwa dakiak 3 sekunde 29.73.

Bingwa wa Jumuia ya Madola Ferdinand Omanyala, alichukua nafasi ya tatu kwa mara nyingine tena kwa muda wa sekunde 10.01.

Mmarekani Trayvon Brommell, alitwaa ushindi kwa kuweka muda wa kasi ulimwenguni mwaka huu wa sekunde 9.84, akifuatwa na Emmanuell Eseme, kutoka Cameroon kwa sekunde 9.99 .

 

Share This Article