Charles Kamau Karondo ateuliwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CA

Tom Mathinji
1 Min Read
Mary Wambui Mungai, ateuliwa Mwenyekiti asiye na mamlaka wa Bodi ya Wakurugenzi ya CA.

Rais William Ruto, amemteua Charles Kamau Karondo, kuwa Mwenyekiti asiye na Mamlaka wa Bodi ya Wakurugenzi ya Halmashauri ya Mawasiliano Nchini (CA).

Kwenye Gazeti Rasmi la Serikali chapisho la Agosti 8, 2025, Rais alisema Karondo atahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu, huku uteuzi huo ukianza kutekelezwa mara moja.

Uteuzi wake unachukua mahala pa mfanyabiashara Mary Wambui Mungai, ambaye uteuzi wake umebatilishwa.

Katika Gazeti Rasmi hilo la Serikali, Waziri wa Maji, Usafi na Unyunyizaji mashamba maji Eric Mugaa, amemteua  Mary Wambui kuwa mwenyekiti asiye na mamlaka wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Maji ya Adhi kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu.

Wambui amechukua wadhifa huo kutoka kwa Karondo ambaye uteuzi wake ulibatilishwa.

Share This Article