CHAN 2024: Waganda wahitaji sare kuvuka mto Nile

Mchuano huo wa nne kwa timu zote mbili utang’oa nanga saa mbili usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa michuano ya CHAN, Uganda Cranes, watashuka dimbani Namboole leo Jumatatu jioni kupimana ubabe na Bafana Bafana ya Afrika Kusini, huku sare ya aina yoyote ikitosha kuwavusha Waganda hadi robo fainali.

Mchuano huo wa nne kwa timu zote mbili utang’oa nanga saa mbili usiku.

The Cranes wanaongoza kundi hilo kwa alama 6 wakifuatwa na Algeria na Afrika Kusini kwa pointi 5 kila moja, nao Guinea ambao tayari wamebanduliwa mashindanoni wana alama 4, huku Niger wakivuta mkia kwa  alama 1.

Algeria watachuana na Niger kuanzia pia saa mbili katika uwanja wa Nyayo.

The Dessert Foxes, wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya robo fainali.

Algeria bado watafuzu kwa robo fainali iwapo watatoka sare endapo pia Uganda na Afrika Kusini watatoka sare.

Share This Article