Madagascar watalenga kujikatia tiketi ya robo fainali ya kombe la CHAN leo usiku watakapokwangurana na Burkina Faso katika mechi ya mwisho ya kundi B,uwanjani Amaan kisiwani Zanzibar kuanzia saa mbili usiku.
Madagascar ni sharti wapate ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Burkina Faso, ili kumaliza katika nafasi ya pili kundini humo na kufuzu kwa hatua ya nane bora.
Hata hivyo, Madagascar, walio na alama 4, watakuwa na kibarua kigumu kutoka kwa Burkina Faso, ambao tayari wameyaaga mashindano na watakuwa wakihitimisha tu ratiba.
Mauritania inashikilia nafasi ya pili kwa alama 7, na watafuzu kwa robo fainali endapo Madagascar watashindwa au kwenda sare na Burkina Faso.
Wenyeji wenza wa kipute cha CHAN, Tanzania, watakamilisha ratiba dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati uwanjani Benjamin Mkapa kuanzia saa mbili usiku.
Tanzania maarufu, Taifa Stars, wameshinda mechi zote tatu wakiwa na alama 9 wakiwa tayari wamefuzu kwa robo fainali