Harambee Stars itachuana na Madagascar katika robo fainali ya kwanza ya kipute cha Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN) Ijumaa hii.
Kenya ilifuzu baada ya kungoza kundi A kwa alama 10, moja zaidi ya Morocco waliomaliza nafasi ya pili.
Kenya walifuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza, wakishiriki kwa mara ya kwanza baada ya kuwalaza Zambia goli moja kwa bila katika mechi ya mwisho iliyosakatwa katika uwanja wa Kasarani Jumapili alasiri.
Morocco walioiparamia DRC mabao 3-1, watatembea Dar es Salaam, Tanzania, kupambana na wenyeji Ijumaa usiku.