CHAN 2024: Mashetani wa Congo wanusurika kutafunwa na mamba wa Sudan

Ilikuwa mara ya tano kwa Congo, kuepuka kushindwa katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya CHAN.

Dismas Otuke
1 Min Read

Congo walinusurika kichapo dhidi ya Sudan katika pambano la kundi D kuwania kombe la CHAN leo jioni katika uwanja wa Amaan, kisiwani Unguja.

Musa Hussien aliwaweka vijana wa Kwesi Appiah, Sudan, uongozini katika dakika ya 29, kabla ya Carly Ekongo, kusawazisha dakika ya 86.

Ilikuwa mara ya tano kwa Congo, kuepuka kushindwa katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya CHAN.

Sudan watakabiliana na Nigeria Agosti 12, huku Congo wakiwa na mtihani mgumu dhidi ya mabingwa watetezi Senegal.

Share This Article