Chameleone atamani kurejelea kazi

Alichapisha video ya awali akiwa jukwaani.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki nguli wa Uganda anayeugua Jose Chameleone amedhihirisha kwamba anatamani kurejelea kazi yake kama mwanamuziki.

Chameleone ambaye yuko Marekani tangu Disemba 2024 kwa ajili ya matibabu alichapisha video ya tumbuizo lake la miezi saba iliyopita katika hoteli ya Africana jijini Kampala.

Wakati huo kakake mdogo Douglas Mayanja maarufu kama Weasel Manizo ambaye pia ni mwanamuziki alikuwa ameandaa tamasha huko lililokuwa likiitwa, “Memories of Goodlyfe”.

Kwenye video hiyo ya zamani, Chameleone ambaye ana matatizo ya kongosho alionekana akiwa na nguvu sawa akitumbuiza jukwaani.

Chini ya video hiyo aliandika, “Insha Allah K.A.T.U.P.A.K.A.S.E” Insha Allah ikimaanisha kwa mapenzi ya Mungu na Katupakase likiwa jina la wimbo wake linalomaanisha tuungane.

Huku hayo yakijiri, mkali wa muziki nchini Tanzania TID naye amemtakia afueni ya haraka rafikiye na mwanamuziki mwenza Jose Chameleone.

Alichapisha picha yao ya pamoja ya awali kwenye Instagram na kuandika, “TBT: 2023 back in Kampala with my Mentor Jose chameleone. Allah akupe afueni ya haraka turejelee kazi tuwanyamazishe Watoto Wadogo…..”

Tayari Chameleone amefanyiwa upasuaji wa kongosho na anaendelea kupata nafuu.

Share This Article