Chama cha ODM kinaadhimisha miaka 20 katika kaunti ya Busia

Tom Mathinji
1 Min Read
Chama cha ODM kinaadhimisha miaka 20 tangu kubuniwa.

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), leo ijumaa kinaadhimisha miaka 20, katika sherehe inayoandaliwa katika shule ya msingi ya Bukiri, eneo la Funyula kaunti ya Busia.

Sherehe hizo zinaongozwa na kinara wa chama hicho Raila Odinga,ambaye hivi majuzi aliwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC, addis Ababa nchini Ethiopia.

Raila alisema kwa sasa anashauriana na wadau mbali mbali kuhusu mwelekeo wake wa kisiasa, baada ya kushindwa kwenye uwaniaji huo wa kiti cha AUC.

“Haya ni mashauriano na watu wetu, hasaa baada ya kile kilichotokea Addis Ababa,” alisema  Raila huku akiashiria uwezekano kujiunga na muungano wa kisiasa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Siku ya Alhamisi, Raila aliandaa mkutano wa mashauriano katika kaunti ya Migori, aliko shauriana na vijana wa chama hicho akiwemo mwanaharakati wa kisiasa Kasmuel McOure.

Alipotangaza atawania uenyekiti wa Tume ya AUC, Raila aliacha wadhifa wa kinara wa ODM, huku Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o akiteuliwa kaimu kiongozi wa chama hicho.

TAGGED:
Share This Article