CHADEMA: Yuko wapi Tundu Lissu?

Tom Mathinji
2 Min Read

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinaitaka serikali ya Tanzania kuelezea aliko kiongozi wake Tundu Lissu, siku mbili baada ya kutiwa nguvuni alipohudhuria mkutano wa hadhara katika eneo la Mbinga, Ruvuma.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Ali Ibrahim Juma, mawakili, familia na wanachama wamedai kuwa licha ya kufika katika gereza za Keko jijini Dar es Salaam ambako Lissu anazuiliwa, hawajapata fursa ya kumwona kiongozi wao, wakifahamishwa na wasimamizi wa gereza hilo kuwa hashikiliwi hapo.

Ni kwa msingi huu ndiposa CHADEMA, kimezitaka mamlaka husika nchini humo kutoa taarifa kwa umma kueleza aliko kiongozi huyo wa upinzani.

Tundu Lissu alikamatwa siku ya Jumatano baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara Mbinga, Ruvuma, lakini sababu za kukamatwa kwake hazikutolewa.

“Hadi sasa sababu halisi za kukamatwa kwake bado hazijawekwa wazi,” ilisema taarifa ya chama hicho kupitia mtandao wa X siku ya Jumatano.

Kukamatwa kwa Lissu kunajiri siku chache baada ya Tume ya Uchaguzi nchini humo, kukipiga marufuku Chama cha CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Tume huru ya Kitaifa ya  Uchaguzi ya Tanzania (INEC), ilitanga kuwa hatua ya kukifungia nje CHADEMA, ilitoka na kukosa kwa chama hicho kutia saini kanuni za Maadili ambao wakati wake umepita.

“Chama chochote ambacho hakukitia saini Kanuni za Maadili, hakitaruhusiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu,” ilisema tume hiyo.

Share This Article